IQNA

Wachezaji wa Man U, Pogba na Diallo wabainisha uungaji mkono wao kwa Palestina

18:17 - May 19, 2021
Habari ID: 3473926
TEHRAN (IQNA)- Paul Pogba nyota wa timu ya soka ya Manchester United ya Uingereza na mwenzake Ahmad Diallo jana walionekana wakiwa na bendera ya Palestina kwa ajili ya kuonyesha uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina wanaokabiliwa na hujuma na ukatili utawala bandia wa Israel.

Tukio hilo lilitokea baada ya kumaliza mechi kati ya Manchester United na Fulham katika Uwanja wa Old Trafford ambapo timu mbili hizo zilitoka sare ya 1-1.

Wachezaji hao ambao wote ni Waislamu wameungana na wachezaji na wapenda haki wengine kote ulimwenguni ambao wamekuwa wakionyesha kwa namna mbalimbali himaya na uungaji mkono wao kwa Wapalestina.

Poga ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, na Diallo anayechezea timu ya taifa ya Ivory Coast walizinguka uwanja wa Old Trafford ambao ulikuwa na mashabiki 10,000. Jana ilikuwa mara ya kwanza kwa mashabiki kuruhusiwa kuingia ugani hapo tokea janga la COVID-19 lianze.

"Tuombeeni Palestina", Pogba aliandika katika ukurasa wake wa Instagram na maandihi hayo yaliambatana na picha iliyomuoneysha akiwa amebeba bendera ya Palestina.

Akizungumzia kuhusu tukio hilo baada ya mechi, Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjae amesema: "Tuna wachezaji kutoka mila na desturi mbali mbali na pia kutoka nchi mbali mbali na hivyo tunapaswa kuheshimu mitazamo yao hata kama itatafautiana na ya wengine."

Ameongeza kuwa: "Iwapo wachezaji wangu wanafikiria kuhusu mambo mengine zaidi ya soka, basi hilo ni jambo chanya."

3474773

captcha