IQNA

Mchezaji wa Liverpool, Mohammad Salah, asoma Qur’ani akiwa safarini kuelekea Kenya

19:10 - March 24, 2021
Habari ID: 3473758
TEHRAN (IQNA) – Mchezaji maarufu wa soka wa timu ya Ligi Kuu ya England, Mohammad Salah ameonekana akisoma Qur’ani Tukufu akiwa ndani ya ndege.

Kwa mujibu wa gazeti la Masri Times, Mohammad Salah ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri, alikuwa ndani ya ndege akielekea nchini Kenya Jumanne ambapo picha yake akisoma Qur’ani Tukufu ndani ya ndege imeenea katika mitandao ya kijamii.

Timu ya Taifa ya Misri inatazamiwa kucheza na Timu ya Taifa ya Kenya Alhamisi katika mechi ya kuwani kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2021.

Mchezaji huyu ni Mohammad Salah ni maarufu kwama 'Mfalme wa Misri' na ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji bora katika Ligi Kuu ya Uingereza hivi sasa na ana wafuasi wengi ambao wanavutiwa na kipaji chake na pia kufungamana kwake na mafundisho ya Kiislamu. Idadi kubwa ya mashabiki wa Liverpool wameweza kuvutiwa na Uislamu kutokana na maadili bora ya Salah ambaye ametajwa kuwa mfano wa kuigwa.

Mbali na kusoma Qur’ani,  Salah pia mepata umaarufu kwa kusoma Duaa kabla ya mechi na pia wakati mwingi husujudu baada ya kufunga bao.

Halikadhalika Salah pia anahusika na miradi kadhaa ya kusaidia jamii kama vile kujenga shule nchini Misri na hivyo amekuwa ni kigezo kwa vijana wengi Waislamu duniani.

3961087

captcha