IQNA

Ahlul Bayt AS

Bendera ya Fatemi yapandishwa katika Chuo Kikuu cha Islamabad kwa mnasaba wa kufa shahidi Bibi Fatima Zahra (SA)

20:03 - December 06, 2024
Habari ID: 3479862
IQNA - Kuashiria kumbukumbu ya kifo cha kishahidi cha Bibi Fatima Zahra (SA), bendera ya Fatemi ilipandishwa katika hafla ya maombolezo katika Chuo Kikuu cha Al-Kawthar huko Islamabad, Pakistan.

Ujumbe kutoka Haram ya Hadhrat Abbas (AS) nchini Iraq ulihudhuria hafla hiyo.

Wakati huo huo, Karachi kusini mwa Pakistani imepangwa kuandaa programu kwa ajili ya wanawake chini ya kauli mbiu "Njia ya Hadhrat Zahra (SA) ni Njia ya Wokovu".

Mpango huo utafanyika kwa muda wa siku saba na kwa himaya ya Taasisi ya Turath al-Anbiya yenye uhusiano na Idara y Mfawidhi wa Haram ya Hadhrat Abbas (AS).

Kwa mujibu wa Sheikh Nassir Abbas Najafi, mwakilishi wa idara hiyo,, itajumuisha shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na semina, usomaji wa mashairi, na hotuba juu ya Siira ya Hazrat Zahra (SA).

Inalenga kufafanua vipengele tofauti vya Siera ya binti mpenzi wa Mtukufu Mtume (SAW).

Waislamu wa madhehebu ya Shia na wengine katika sehemu mbalimbali za dunia hushiriki katika hafla kila mwaka ifikapo siku ya tatu ya mwezi wa Jumada al-Thani katika kalenda ya mwandamo ya Hijri kuomboleza kumbukumbu ya kufa shahidi Bibi Fatima Zahra (SA), binti kipenzi cha Mtume Muhammad (SAW).

3490943

 

Kishikizo: Fatima Zahra
captcha