Kituo cha Qur'ani cha Wanawake, chenye uhusiano na Idara ya Mfawidhi wa Haram takatifu ya Hadhrat Abbas (AS) kiliandaa programu hizo katika Kituo cha Al-Barakia wiki iliyopita.
Ilijumuisha usomaji wa pamoja wa Surah Al-Fajr ya Qur’ani Tukufu.
Kulikuwa pia na usomaji wa Dua ya Faraj pamoja na vikao vya maombolezo na qiraa ya Qur’ani, kwa mujibu wa Manar al-Jabouri, mkuu wa Kituo cha Qur'ani cha Wanawake.
Alisema programu hizo zinalenga kuongeza uelewa wa kidini miongoni mwa wanawake na kuhifadhi turathi za kidini.
Shughuli hizo pia husaidia kukuza mapenzi kwa Ahl-ul-Bayt (AS) na kuimarisha maadili ya kidini na ya kibinadamu katika jamii, alibainisha.
3490737