Usiku wa kwanza wa ibada za maombolezo ya kuadhimisha tukio hilo la kusikitisha ulifanyika katika ukumbi wa kidini Husseiniya ya Imam Khomeinimjini Tehran Jumatatu jioni.
Idadi kubwa ya waumini na wafuasi wa Ahl-ul-Bayt (AS), wakiwemo maafisa wakuu mfumo wa Kiislamu Iran na wananchi wa tabaka tofauti walishiriki katika hafla hiyo.
Ilianza kwa usomaji wa aya za Quran Tukufu na qari mashuhuri wa Iran Hadi Movahed Amin.
Kisha, Hujjatul Islam Mehdi Aslani alitoa hotuba ambayo ndani yake alifafanua juu ya "uhandisi wa Tabyeen (ufafanuzi)" kwa kuzingatia aya za Qur’ani kama moja ya sifa za Hazrat Zahra (SA).
Amesema Qur'ani inazingatia njia ya mapambano na muqawama kuwa inawezekana tu kwa kuzingatia imani ya akhera.
Katika mjumuiko huo wa maombolezo, msoma mashairi ya maobolezo Saeed Haddadian alisoma tungo za maombolezo ya Bibi Fatimat Zahra (SA).
Waislamu wa madhehebu ya Shia na wengine katika sehemu mbalimbali za dunia hufanya ibada kila mwaka ifikapo siku ya tatu ya mwezi wa Jumada al-Thani katika kalenda ya mwandamo ya Hijri kuomboleza kumbukumbu ya kuuawa shahidi Bibi Hadhrat Zahra (SA), binti kipenzi cha Mtume Muhammad (SAW).
3490921