IQNA

Ahul Bayt AS

Kuzaliwa kwa Kawthar: Bibi Zahra na Surah Al-Kawthar

16:21 - December 22, 2024
Habari ID: 3479936
IQNA – Katika Sura Al-Kawthar ya Qur'ani Tukufu, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemneemesha Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) kwa kumpa “Kawthar,” ili kuinua roho yake na kubainisha kuwa wale wanaomsema vibaya ni wao wenyewe watakaosalia bila ya vizazi.

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (SAW) alimuoa Bibi Khadijah (SA) alipokuwa na umri wa miaka thelathini, na ndoa hii ilibarikiwa kwa watoto kadhaa. Mmoja wa watoto hawa ni Fatimah Zahra (SA), ambaye kuzaliwa kwake kwa baraka kulitokea mwaka wa tano baada ya Bi’tha (kuteuliwa kuwa Utume).

Wakati huu, hasa katika mwaka wa nne na wa tano baada ya Bi'tha, wakati mwaliko wa Mtume Muhammad (SAW) ulipodhihirika na Maquraishi wakazidisha upinzani wao dhidi yake na kufuatiwa na kuaga dunia kwa wana wa Mtume, Qassim na Abdullah. Msiba huu ulipelekea maadui zake wafurahi sana. Walitangaza kwamba hatakuwa tena na kizazi. Al-As ibn Wa’il, mmoja wa waliokuwa wakimdhihaki Mtume wa Mwenyezi Mungu, alichukua fursa iliyoletwa na vifo vya wana wa Mtume (SAW) kumwita “Abtar”, kumaanisha bila ya kizazi.

Waarabu hawakuwathamini mabinti na hawakuwaona kuwa ni sehemu ya nasaba yao. Tusi hili kutoka kwa Al-As ibn Wa’il lilienea haraka na sio tu kwamba liliumiza moyo mtukufu wa Mtume (SAW) bali pia liliacha athari mbaya kwa ari ya Waislamu.

Katika hali hiyo Qur'ani Tukufu ikawa faraja kwani ilimfarjiji na kumfariji na kumtuliza Mtukufu Mtume Muhamamd (SAW), ikizungumzia propaganda mbaya za Maquraishi. Surah Al-Kawthar iliteremshwa kwa ajili hii. Katika Sura hii, Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa rehema Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW), akisema kwamba amempa "Kawthar", ili kuinua roho yake na kumfanya aelewe kwamba wale wanaomsema vibaya ndio hatimaye kuwa bila vizazi.

Mwenyezi Mungu anasema katika Surat A-Kawthar:

“Hakika sisi tumekupa wewe (Mtume Muhammad) Kawthar (Kheri Nyingi).

Basi mwabudu Mola wako Mlezi na utoe sadaka.

Hakika adui yako ndiye asiye na kizazi.”

Mfasiri mkuu wa Qur'ani Fakhr al-Razi anaifafanua Sura hii kwa kusema. “Maana ya sura ni kwamba Mwenyezi Mungu anamjaalia Mtume nasaba ambayo itadumu. Fikiria ni wangapi wa familia yake waliuawa, hata hivyo dunia imejaa dhuria wa Mtume wa Allah SAW na hakuna yeyote kutoka katika familia ya Umayya anayeweza kulinganishwa naye katika suala hili. Pia, zingatia jinsi wanachuoni wakubwa walivyotokea kutoka kwenye ukoo wa Mtume, kama vile Baqir, Sadiq, Kadhim, Reza, na Nafas Zakiyah."

Mtoto ambaye kupitia kwake ukoo wa Mtume Muhammad (SAW) uliendelea alikuwa ni Fatimah Zahra (SA). Baada ya kuolewa na Ali ibn Abi Talib (AS), alikuja kuwa mama wa watoto kama vile Hassan na Hussein (AS), ambao ni viongozi wa vijana wa Peponi. Hata hivyo, binti huyu mtukufu wa Mtume (SAW) alikuwa na maisha mafupi na alijiunga na baba yake mtukufu miezi mitatu au sita baada ya kufariki Mtume, katika mwaka wa kumi na moja baada ya Hijra.

Ikumbukwe kuwa leo ni Jumapili 20 Mfunguo Tisa Jamadithani 1446 Hijria, mwafaka na 22 Disemba 2024 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 1454 iliyopita kwa mujibu wa kalenda ya Hijria, alizaliwa Bibi Fatima Zahra, binti mtukufu wa Mtume Muhammad (SAW). Bibi Fatima Zahra alilelewa katika nyumba ya wahyi na chini ya malezi bora na mwongozo wa baba yake Mtume Muhammad (SAW) na hivyo kuweza kufikia daraja za juu za ukamilifu. Bibi Fatima (AS) alikuwa na nafasi kubwa katika kukabiliana na matatizo na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikimkabili baba yake kutoka kwa washirikina. Mwaka wa pili Hijiria, Bibi Fatima Zahra alifunga ndoa na Imam Ali bin Abi Twalib (AS) ambaye ni dhihirisho la haki, uadilifu na uchaji-Mungu katika sherehe ndogo iliyosimamiwa na Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Vilevile Bibi Fatima akiwa na Imam Ali alifanikiwa kulea shakhsia adhimu kama Hassan, Hussein na Bibi Zainab (AS). Mbali na majukumu ya kulea familia, Bibi Fatima Zahra, alijishughulisha pia na malezi ya jamii.

3491142

captcha