Kituo cha Telegram cha Sabereen News kilichapisha picha zinazoonyesha watu wenye silaha wakipora eneo hilo takatifu.
Hayo yamejiri wakati ambapo makundi ya wanamgambo walioingia Damascus baada ya kuanguka kwa serikali ya Rais Bashar al-Assad walikuwa wameahidi kwamba hakutakuwa na vitendo vya kuvunjia heshima eneo hilo takatifu.
Wanamgambo, wakiongozwa na kundi Hay’at Tahrir al-Sham (HTS), walitangaza amri ya kutotoka nje Damascus siku ya Jumapili hadi asubuhi iliyofuata, baada ya kuuteka mji mkuu kufuatia mashambulizi ambayo yamepelekea kuondolewa madarakani Bashar Al Assad
Abu Mohammad al-Jolani, kamanda wa HTS, alisema Jumapili kwamba taasisi za serikali ya Syria zitasimamiwa na Waziri Mkuu wa serikali ya Assad, Mohammad Ghazi al-Jalali hadi mpito wa madaraka ufanyike.
HTS ilisema itafanya kazi na waziri mkuu na kutoa wito kwa vikosi vya jeshi la Syria huko Damascus kutohujumu taasisi za umma.
Assad aliripotiwa kuondoka Syria kwa ndege mapema jana mchana, na kuhitimisha zaidi ya miongo mitano ya utawala wa familia yake juu ya Syria.
3490984