Siku ya Jumatano usiku, mtandao wa KHAMENEI.IR ulichapisha ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa lugha ya Kiingereza kama ifuatavyo: “Kama Yesu (as) angekuwa miongoni mwetu hii leo, asingesitasita hata kidogo kupambana na viongozi wakandamizaji na mabeberu wa dunia ya leo, na wala asingestahamili njaa na kulazimishwa kuhama kwa mabilioni ya watu ambao wamesukumwa vitani na madola ya kibeberu.
Jana Jumatano, tarehe 25 Desemba 2024, iliadhimishwa na Wakristo kama sikukuu ya Krismasi ambayo ni maadhimisho ya kuzaliwa Yesu Kristo au Nabii Isa mwana wa Mariam (Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-AS-).
Katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuna idadi ndogo ya Wakristo ambao wana haki kuabudu na hivyo waoa nao pia huadhimisha siku hii katika miji mbalimbali.
Mtukufu Isa Masih (AS), ambaye ametajwa katika Qur'ani Tukufu kama Ruhullah, ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwana wa Bibi Maryam (AS).
4256258