Katika ujumbe wa pongezi kwa Papa Francis, kiongozi wa Wakatoliki duniani, kwa mnasaba wa Sikukuu ya Krismasi ambayo ni maadhimisho ya kuzaliwa Yesu Kristo au Nabii Isa mwana wa Mariam (Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake) na kuanza Mwaka Mpya wa 2025, Rais Masoud Pezeshkian amesema: "Katika zama za sasa, jamii inahitaji mtazamo mpya wa kutatua masuala ya jamii za binadamu, hivyo kufikiria na kutafakari juu ya sifa kuu za manabii wa Mungu kunaweza kuwa njia ya kufanikisha ukamilifu wa binadamu wa kisasa.
Katika ujumbe huo, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza matumaini yake kwamba katika siku hizi za kuelekea kwenye mwaka mpya wa Miladia, tutashuhudia hatua madhubuti katika njia ya kufikia amani, usalama na uhuru wa mataifa yaliyodhulumiwa na wanyonge, hasa watu wanaokandanizwa wa Palestina.
Jana Jumatano tarehe 25 Disemba, kwa mujibu wa maandishi ya Kikristo, ilikuwa siku ya kukumbuka kuzaliwa Nabii Isa Masih (AS) ambaye alizaliwa katika mji wa Bait Laham (Bethlehem) huko Palestina, miaka 2024 iliyopita.
Nabii Isa Masih alipewa uwezo na Mwenyezi Mungu wa kufanya miujiza mingi. Isa Masih AS alianza kuzungumza akiwa mdogo na kujibashiria Unabii.
Inafaa kuashiria hapa kwamba, tarehe 25 Disemba kila mwaka inajulikana kote duniani hasa kwa Wakristo kuwa ni Sikukuu ya Krismasi.
4256155