Musa Akram Nuais aliambia IQNA, pembeni mwa mashindano hayo kuwa kusoma na kutafakari aya za Qur’ani Tukufu ni muhimu, na baadaye aya hizo zinapaswa kutekelezwa katika maisha ya kila siku.
Alisema alianza kuhifadhi Qur’ani Tukufu akiwa na umri wa miaka 8 katika Haram ya Imam Hussein (AS) huko Karbala, na alifanikiwa kuhifadhi Qu’rani yote akiwa na miaka 13.
Teknolojia Mpya Katika Kuhifadhi Qur’ani Tukufu
Alipoulizwa kuhusu matumizi ya teknolojia mpya na ubunifu katika kuhifadhi Quran Tukufu, alisema kuwa kwa asili, kuhifadhi Quran kunahitaji kuisikiliza na kuirudia mara kwa mara, jambo ambalo linaanzisha mchakato wa kuhifadhi.
"Kwa hakika, matumizi ya nyenzo mpya katika kuhifadhi Qu’rani yanaweza kuwa na manufaa, lakini bado tunahitaji walimu wenye uzoefu ili kuhakikisha kuwa Quran inahifadhiwa kwa usahihi," aliongeza.
Mchango wa Familia Katika Kuhifadhi Qur’ani
Nuais pia alieleza jinsi familia yake ilivyomsaidia katika safari yake ya kuhifadhi Qur’ani, akisema:
"Nililelewa katika familia inayozingatia Qur’ani. Ndugu zangu watatu pia ni wahifadhi wa Qur’an, na mama yangu amehifadhi Qur’an yote pia. Niliihifadhi Qur’ani pamoja nao, na kwa kawaida, mazingira ya familia yetu yaliunga mkono uhifadhi wa Qur’ani Tukufu."
Wasomaji wa Qur’ani Tukufu anaowapenda
Alipoulizwa kuhusu wasomaji maarufu wa Qur’ani aliowachukua kama mifano, alisema:
"Ninasikiliza usomaji wa wasomaji wengi, lakini kwa mfano, ninapendelea usomaji wa qari mashuhuri wa Misri aliyefariki Ustadh Minshawi. Miongoni mwa wasomaji wa Iraq, ninafurahia usomaji wa Osama Al-Karbalayi, Maytham al-Tammar, na wengineo."
Maoni Kuhusu Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran
Alipozungumzia mashindano ya kimataifa ya Qur’ani yanayoandaliwa na Iran, alisema kuwa inajulikana wazi kuwa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani yanayoandaliwa na Iran ni miongoni mwa mashindano yenye hadhi kubwa zaidi duniani.
"Iran imekuwa ikiandaa mashindano haya ya Qu’rani kwa zaidi ya miaka 40, ikizingatia sana uteuzi wa washiriki na majaji. Mchakato wa uamuzi na utendaji wa washiriki pia unachunguzwa kwa makini," alisema.
liendelea kusema kuwa mashindano kama haya yana nafasi kubwa katika kuhamasisha kizazi kipya kuhifadhi Qu’rani na kuwasaidia kufikia viwango vya juu katika uwanja huu.
"Pia yanawahamasisha kutamani kufikia kiwango cha wale wanaoshiriki katika mashindano haya."
ashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran
Wasomaji na wahifadhi wa Qur’ani kutoka nchi 144 walishiriki katika raundi za awali za Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya 41 ya Iran, na kutoka kwao, wawakilishi kutoka nchi 27 wamefika hatua za fainali katika vipengele vya wanaume na wanawake.
ainali hizo, ambazo zinafanyika katika mji mtakatifu wa Mashhad, kaskazini-mashariki mwa Iran, zitafikia tamati Ijumaa katika hafla ya kufunga ambapo washindi wakuu watatangazwa na kutuzwa.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huandaliwa kila mwaka na Shirika la Awqaf na Masuala ya Hisani la nchi hiyo.
Lengo lake ni kukuza tamaduni na maadili ya Qur’ani Tukufu miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi wa Qur’ani Tukufu.