IQNA

Mufti wa Tunisia aomba radhi kwa kutangaza Idi mapema

12:33 - July 20, 2015
Habari ID: 3330378
Mufti wa Tunisia Sheikh Hamda Saeed amewaomba radhi Watunisia baada ya kubaini kuwa alifanya kosa kwa kutangaza mapema siku kuu ya Idul Ftir.

Kwa mujibu wa televisehni ya Al-Alam, mufti huyo alihutubia taifa Alhamisi na kulitangazia taifa la Tunisia kuwa Idul Fitr itaadhimishwa Ijumaa, Julai 17. Hatahivyo baadaye Sheikh Saeed alikiri kosa lake na kusema Idul Fitr ilikuwa Jumamosi na wala si Ijumaa kama alivyokuwa ametangaza.
“Kulikuwa na kosa katika kuuona Mwandamo wa Mwezi wa Shawwal na nilifanya kosa kutangaza Idi kuwa Ijumaa,” amesema. “Nawaomba radhi watu wa Tunisia, hasa Waislamu…kwa kosa hili,” ameongeza.
Siku ya Ijumaa  baadhi ya nchi za Kiislamu ziliadhimisha Siku Kuu ya Idul Fitr kwa kutegemea tangazo la Saudi Arabia kuhusu kuandama mwezi.
Hatahivyo baadhi ya nchi za Kiislamu kama vile Iran, Oman, Afghanistan na pia nchi za Afrika Mashariki kama vile Kenya na Tanzania zilitangaza Ijumaa kuwa siku ya 30 ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Ijumaa kuwa tarehe Mosi Shawwal na Siku Kuu ya Idul Fitr.../mh

3330215

captcha