IQNA

Baraza la Fatwa Ulaya

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuanza Juni 18 barani Ulaya

14:32 - June 06, 2015
Habari ID: 3311365
Barani Ulaya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unatazamiwa kuanza Alkhamisi Juni 18. Tangazo hilo limetolewa na Baraza la Fatwa na Utafiti Ulaya (EFCR) kwa mujibu wa mahesabu ya kifalaki.

“Hilali ya Ramadhani itazaliwa  Jumanne, Juni 16, 2015 saa 14:05 GMT (17:05 alasiri kwa saa za Makkah),” imesema taarifa ya baraza hilo lenye makao yake huko Dublin nchini Ireland.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, itakuwa haiwezekani kuona mwezi mwandamo wakati wa Magharibi Jumatano, Juni 17, kwa jicho au hata kwa suhula za kisasa kama vile telescope.
Kwa msingi huo, “Alkhamisi Juni 18 itakuwa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kwa idhini yake Allah SWT.”
Kwingineko Jumuiya ya Kiislamu ya Amerika Kaskazini (ISNA) nayo pia imetangaza kuwa, kwa mujibu wa taarifa za wataalamu , Juni 18 itakuwa tarehe mosi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika mwaka huu wa 1436 Hijria.../mh

3311251

captcha