IQNA

Zaidi ya asilimia 67 ya Waislamu Marekani wameshuhudia chuki dhidi ya Uislamu

22:48 - October 01, 2021
Habari ID: 3474368
TEHRAN (IQNA) – Uchunguzi mpya umebaini kuwa zaidi ya asilimia 67.5 ya Waislamu wanaoishi Marekani wamekumbana na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu (Islampohobia) walau mara moja maishani.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha California, Berkeley, wanawake ndio waliokumbwa na vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu zaidi ya wanaume. Wanawake waliokumbana na Islamophobia ni asilimia 76.7 ikilinganishwa na wanaume ambao ni asilmia 58.6.

Uchunguzi huo umebaini kuwa asilimia 33 ya Waislamu wa Marekani wamelazimika kuficha imani yao katika baadhi ya nyakati kwa kuhofia kuhujumiwa au kubaguliwa na wenye chuki dhidi ya Uislamu huku asilimia 88.2 wakisema walijepusha kutamka maneneo au kuchukua baadhi ya hatua kwa hofu ya kushambuliwa kutokana na imani yao.

Halikadhalika asilimia 93.7 ya Waislamu Marekani wanasema vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu huathiri hisia zao na afya ya kiakili.

Uchunguzi huo umefanyika miongo miwili baada ya hujuma za Septemba 11 nchini Marekani ambazo zilisbabaisha ongezeko kubwa  vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu ambavyo vimewalenga mamillioni ya Waislamu Marekani.

/3475855

captcha