IQNA

Hujuma dhidi ya kituo cha Kiislamu cha Chuo Kikuu cha Rutgers Marekani

20:40 - April 12, 2024
Habari ID: 3478675
IQNA-Wanafunzi wa aislamu katika Chuo Kikuu cha Rutgers nchini Marekani wameelezea wasiwasi juu ya usalama wao baada ya kituo chao cha Kiisilamu kuharibiwa wakati wa siku kuu ya Idul Fitr.

Hali ya wasiwasi imetanda miongoni mwa wanafunzi wa Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Rutgers kufuatia uharibifu wa Kituo cha Kiislamu cha chuo kikuu, jinai ambayo iliambatana na sikuukuu ya Idul Fitr baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika onyesho la mshikamano, wanafunzi wasiokuwa Waislamu walikusanyika kwa lengo la kubainisha mshikamano na pia  msaada kwa wanafunzi wa Waislamu katika Kituo cha Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Rutgers.

Kiongozi wa Wakristo chuoni hapo Matt Murphy alionyesha kufadhaika kwake, akisema, "Nadhani inashangaza kile kilichotokea hapa. Kitendo hiki ni kibaya. Kwa hivyo tunashikamana na Waislamu­­­. "

Nehad Ali, mwanafunzi, alibainisha wasiwasi wake, akisema, "Eneo letu salama hapa limevurgwa wakati wa Idi, na bendera yetu ya Palestina ilichukuliwa, na huo ni ujumbe ambao tumefikishiwa."

Taaarifa zinasema mbali na wizi wa bendera ya Palestina vipande vya sanaa vilivyopambwa na aya za Qur’an viliharibiwa, na madirisha yalivunjwa.

Nora Asker, rais wa Baraza la Mahusiano ya Umma ya Waislamu Marekani, amekuwa akiwasihi maafisa wa Rutgers  kutoa ulinzi kwa wanafunzi wa Waislamu na Kiarabu, haswa wale wa asili ya Palestina, kwa kuzingatia vita vya Israeli vinavyoendelea dhidi ya Gaza.

Asker alisema, "Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) imekuwa ikisumbua chuo chetu, ikionyesha ubaguzi katika maneno ya wanafunzi.”

Maafisa wa Rutgers wamelaani hadharani tukio hilo katika Kituo hicho, wakithibitisha kujitolea kwao kushughulikia kila taarifa ya chuki dhidi ya Uislamu.

3487902

captcha