IQNA

Mbunge Muislamu Marekani ahujumiwa na wabunge wenzake

19:10 - December 01, 2021
Habari ID: 3474624
TEHRAN (IQNA) – Mbunge Muslamu katika Bunge la Congress nchini Marekani, Bi. Ilhan Omar wa chama cha Democrat amehujumiwa kwa maneno makali na mbunge mwenzake mwenye misimamo mikali wa chama cha Republican ambaye amemtaja kuwa ‘mwenye kiu cha damu’ na mtetezi wa ugaidi.

Marjorie Taylor Green anayewakilisha jimbo la Georgia katika Baraza la Wawakilishi la Marekani ameshiriki katika mdahalo wa televisheni ulioandaliwa na mshauri wa zamani wa Trump, Steve Bannon ambapo ametetea matamshi yaliyotolewa dhidi ya Omar na mbunge mwingine wa chama cha Republican Lauren Boebert.

Katika klipu iliyoenea, Boebert alionekana akimtaja Bi. Omar, raia wa Marekani aliyezaliwa Somalia, kuwa ni mtu ‘muovu’ na  mwenye ‘roho nyeusi.’ Ilhan Omar ni Mwislamu mwenye kufungamana na mafundisho ya dini na ni mwakilishi wa jimbo la Minnesota.

Kwa mujibu wa taarifa, Boebert amelazimika kuomba radhi na kusema ‘naomba msamaha kwa yeyote niliyemkosea katika jamii ya Waislamu.’

Siku ya Jumanne Green alisema ‘Lauren Boebert hakufanya kosa lolote’ huku naye akitoa matamshi yasiyo na msingi kumhusu Omar.

Green amekariri madai ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliyedia kuwa eti Omar anaunga mkono kundi la kigaidi la Al Qaeda.

Kile ambacho Bi. Omar amekuwa akisema ni kuwa sera za kigeni za Marekani zimechangia pakubwa hujuma za kigaidi zinazoshuhudiwa duniani huku akisema jinai wanaoztenda magaidi ni sawa na jinai ambazo zinatenda na Israel na Marekani.

Bi. Omar pia aliwahi kupinga sera za Marekani dhidi ya Iran na kusema vikwazo na vita vya kiuchumi ni hatua ambazo zinakinzana na sera za kupunguza taharuki. Aidha aliwasilisha muswada katika bunge ili  kuziwa kutumiwa nguvu za kijeshi dhidi ya Iran bila idhini ya bunge.

3476747

captcha