IQNA

Jinai za Israel

Israel yawashambulia wavuvi wa Kipalestina katika Pwani ya Gaza

20:50 - September 30, 2023
Habari ID: 3477674
AL-QUDS (IQNA) - Vikosi vya wanamaji vya jeshi la utawala katili wa Israel vimewajeruhi takriban wavuvi wawili wa Kipalestina baada ya kushambulia boti kadhaa katika pwani ya kaskazini ya Ukanda wa Gaza unaozingirwa.

Shambulio hilo lilitokea Jumamosi wakati wavuvi hao walipokuwa wakisafiri kwa mashua ndani ya maili sita kutoka pwani ya Gaza.

Wanaume waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali ya karibu ili kupata matibabu ya haraka.

Wavuvi wa Kipalestina wanakabiliwa na mashambulizi ya Israel karibu kila siku na wale wanaokaribia eneo ambalo utawala ghasibu wa Israel umebaini kuwa eti ni kikomo cha uvuvi hupigwa risasi au kuzuiliwa na jeshi katili la utawala huo.

Israel mara kwa mara huwapiga risasi na kuwaweka kizuizini wavuvi wa Gaza kwa madai ya kuvuka "eneo maalum la uvuvi," ambalo ni takriban maili tatu za baharini.

Chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa kati ya Waisraeli na Wapalestina kufuatia vita vikali vya Israel dhidi ya Gaza mnamo Agosti 2014, Tel Aviv ilikubali kupanua eneo la uvuvi katika pwani ya Gaza, kuruhusu wavuvi wa Kipalestina kusafiri hadi maili sita kutoka pwani. Makubaliano hayo pia yalibainisha kuwa Israel itapanua eneo hilo hatua kwa hatua hadi maili 12.

Hivi sasa, kuna wavuvi wapatao 4,000 katika ardhi ya pwani iliyozingirwa na mamia tu kati yao wanavua mara kwa mara kwani wanahofia kupigwa risasi au kukamatwa na vikosi vya wanamaji vya utawala haramu wa Israel.

Habari zinazohusiana
Kishikizo: jinai za israel gaza
captcha