Shambulio la kikatili la utawala wa Israel dhidi ya shule ya al-Tabi'in katika kitongoji cha al-Daraj katika Jiji la Gaza, ambalo linahifadhi watu waliokimbia makazi yao mashariki mwa Ukanda wa Gaza, liliua zaidi ya raia 100 Jumamosi wakati wa Swala ya alfajiri.
Utawala wa Kizayuni wa Israel ulidai kuwa shambulio hilo liliwalenga wapiganaji wa harakati ya Hamas na Jihad Islami. Katika taarifa Hamas imesema madai hayo kuwa hayana msingi wowote na hayaweza kuhalalsiha wa shambulio hilo la kinyama, na kusisitiza kwamba hakuna hata mtu mmoja mwenye silaha aliyeuawa.
Wote walikuwa raia waliouawa kishahidi walipokuwa wakisali Swala ya Alfajiri, Hamas ilisema.
Walikuwa watoto, wafanyikazi wa serikali, maprofesa wa vyuo vikuu na wasomi wa kidini ambao hawakuwa na jukumu lolote katika shughuli za kisiasa au kijeshi, Hamas ilisisitiza.
Mauaji ya hivi punde ambaye yametekelezwa na utawala katili wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza yamelaaniwa duniani kote.
Ukiungwa mkono na Marekani na waitifaki wake wa Magharibi, utawala ghasibu wa Israel ulianzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza baada ya kukumbwa na Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ya wapigania ukombozi wa Palestina ambao walikuwa wanalipiza kisasi jinai za zaidi ya miongo saba za utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina. Tokea wakati huo, kwa himaya ya Marekani, utawala wa Israel umeua zaidi ya Wapalestina 40,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
3489451