IQNA

Jinai za Israel

Mkuu wa UN: Kinachoendelea Gaza hakikubaliki kabisa

22:16 - September 12, 2024
Habari ID: 3479423
IQNA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alielezea kile kinachotokea katika Ukanda wa Gaza kuwa "hakikubaliki kabisa" baada ya wafanyakazi sita wa Umoja wa Mataifa kuuawa katika shambulio la anga la utawala haramu  wa Israel kwenye shule katika eneo la Palestina.

Antonio Guterres alisema siku ya Jumatano kuwa wafanyakazi sita kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio la bomu la Israel katika shule inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Gaza ya kati.

"Kinachotokea Gaza hakikubaliki kabisa. Shule iliyogeuzwa makazi ya takriban watu 12,000 ilishambuliwa tena na Israel leo," Guterres alisema kwenye X.

"Wenzetu sita wa @UNRWA ni miongoni mwa waliouawa," aliongeza.

Kauli yake imekuja baada ya takriban watu 18 kuuawa Jumatano katika shambulizi la bomu lililofanywa na utawala katili wa Israel dhidi ya shule ya al-Jaouni katika makazi ya raia waliokimbia makazi yao katikati mwa Gaza, na wengine kadhaa kujeruhiwa.

"Ukiukaji huu mkubwa wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu unahitaji kukomeshwa sasa," Guterres alisema.

UNRWA ilisema hii ni "idadi kubwa zaidi ya vifo" kati ya wafanyikazi wake katika tukio moja.

"Miongoni mwa waliouawa ni meneja wa makao ya UNRWA na wafanyakazi wengine wa timu wakitoa msaada kwa watu waliohamishwa. Rambirambi za dhati kwa familia zao na wapendwa," ilisema kwenye X.

Shule hiyo imepigwa mara tano tangu utawala haramu wa Israel uanzishe vita vya mauaji ya kimbari dhdi ya  Gaza Oktoba mwaka jana. Taarifa ya UNRWA imesema : "Shule na miundombinu mingine ya kiraia lazima ilindwe wakati wote. Sio walengwa."

Utawala wa Israel umeendeleza vita vyake vya mauaji ya kimbari  dhidi ya Gaza tangu kundi la Hamas la Palestina lilipotekeleza operesheni ya kulipiza kisasi jinai za Israel mapema Oktoba mwaka jana..

Takriban watu 41,100, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wameuawa na zaidi ya 95,000 kujeruhiwa katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza.

Mashambulizi hayo ya Israel yamewafanya takriban wakazi wote wa eneo hilo kuwa wakimbizi kutokana na mzingiro unaoendelea ambao umesababisha uhaba mkubwa wa chakula, maji safi na dawa.

Israel inakabiliwa na tuhuma za mauaji ya halaiki kwa vitendo vyake huko Gaza katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).

3489870

Habari zinazohusiana
Kishikizo: jinai za israel gaza
captcha