IQNA

Jinai za Israel

Hafidh wa Qur'ani ni miongoni mwa Mashahidi katika moto wa kambi ya hema huko Gaza

10:23 - October 17, 2024
Habari ID: 3479602
IQNA - Shambulio la anga la utawala katili wa Israel kwenye kambi ya hema katikati mwa Gaza mapema wiki hii lilisababisha moto na kuua Wapalestina kadhaa.

Mmoja wa waliouawa kishahidi katika moto huo alikuwa Sahaaban al-Dalw, mhifadhi wa Qur'ani Tukufu, imejitokeza.

Mamake pia aliuawa katika moto huo siku ya Jumatatu.

Video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha waokoaji wakihangaika kuokoa watu walipokuwa wakijitahidi kuzuia moto katika kambi ya hema katika mji wa Deir el-Balah.

 Mhifadhi wa Qur'ani mwenye umri wa miaka 19 alikuwa mwanafunzi wa uhandisi.

Hapo awali alikuwa amerekodi video ambapo alitoa wito kwa walimwengu kuwaunga mkono watu wa Palestina dhidi ya uchokozi wa kikatili wa utawala wa Israel.

Huku kukiwa na utepetevu wa kimataifa, Israel imeshambulia Ukanda wa Gaza bila kuchoka tangu Oktoba 7, 2023, na kuua Wapalestina zaidi ya 42,300, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kuwajeruhi wengine karibu 100,000.

 4242636

captcha