IQNA

Jinai za Israel

Jeshi katili la Israel limeua zaidi ya watoto 15,000 Wapalestina Gaza

18:55 - May 16, 2024
Habari ID: 3478832
IQNA-Zaidi ya watoto 15,000 wanaripotiwa kuuawa shahidi na jeshi la utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.

Hilali Nyekundu ya Palestina imetangaza kuwa, watoto 15,103 wa Kipalestina wameuawa shahidi tangu kuanza hujuma na mashambulio ya kinyama ya utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Ripoti ya Hilali Nyekundu ya Palestina inaashiria pia masaibu makubwa yanayowakabili wanawake wa Kipalestina na watoto hivi sasa kutokana na hali mbaya ya kibinadamu huuko Gaza.

 wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza tangu tarehe 7 mwezi Oktoba 2023 hadi sasa, imeongezeka na kufikia watu elfu 35 na 91 na waliojeruhiwa kufikia elfu 78 na mia 827, ambapo bado unaendeleza mashambulizi ya pande zote na kuua na kujeruhi mamiai ya watu hao wanaodhulumiwa na wasio na ulinzi.

Mauaji haya ya kimbari yanapingwa na kulaaniwa mara kwa mara na mashirika ya kimataifa, hasa Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu kama vile Amnesty International na Human Rights Watch.

 Mbali na mashambulizi ya mabomu na makombora katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza, utawala huo wa Kizayuni unatumia pia silaha ya njaa na kuzuia kufikishwa chakula na dawa

Vitendo vya jinai vya utawala wa Israel huko Gaza hususan mauaji ya kimbari ya watu wa eneo hilo vimeifanya Afrika Kusini ikiwa ni miongoni mwa nchi zinazokosoa jinai za utawala wa Kizayuni kuushtaki utawala huo katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, hatua ambayo imeungwa mkono na makumi ya nchi nyingine za dunia.

4216204

captcha