Tukio hilo la kielimu la kimataifa lililobeba anuani “Kutafsiri Maana za Qur’ani Tukufu: Mbinu, Changamoto na Nafasi ya Teknolojia” lilifanyika kwa njia ya mtandao na kufungwa siku ya Jumamosi.
Washiriki wa mkutano huo walipendekeza kuanzishwa kwa kituo maalumu cha kutafsiri maana za Qur’ani Tukufu kitakachosimamiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Oman.
Kituo hicho kinatarajiwa kuwa jukwaa la kitaifa litakalojishughulisha na kuendeleza kazi za tafsiri, kuunga mkono tafiti za kielimu, pamoja na kuimarisha mafunzo na ushirikiano baina ya watafsiri na watafiti.
Mkutano huo wa siku tatu uliofanyika kwa njia ya mtandao uliandaliwa na Chuo cha Al‑Zahra cha Wanawake kwa ushirikiano na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini. Washiriki walitoa wito wa kuandaliwa kwa zana na viwango madhubuti vya kisayansi vya kupima ubora wa tafsiri, kuchambua sifa za kifasihi za matini ya Qur’ani Tukufu, na kuweka kumbukumbu za maendeleo ya kihistoria ya tafsiri za Qur’ani.
Mapendekezo ya mkutano pia yalisisitiza umuhimu wa kupitia upya tafsiri za zamani kwa kuzingatia maendeleo ya kisasa ya lugha na tamaduni ili kulinda usahihi wa maana. Aidha, ulipendekeza kuanzishwa kwa hifadhidata maalumu na maabara za utafiti zitakazosaidia tafiti za kidijitali za Qur’ani na kuendeleza zana za utafiti wa kisayansi katika uwanja huo.
3496975