IQNA

Msichana wa Gaza apata utulivu na faraja ya kiroho kwa kuhifadhi Qur’ani Tukufu

21:15 - August 01, 2026
Habari ID: 3482567
Habiba Muhammad
IQNA – Wanaharakati kwenye mitandao ya kijamii wamesambaza video yenye kugusa moyo ya msichana mwenye umri wa miaka 12 kutoka Gaza, ambaye kuhifadhi Qur’ani Tukufu kumekuwa kimbilio kwake.

Kwa mujibu wa Al Jazeera, Habiba Muhammad ni mfano wa kuhamasisha wa subira, uthabiti na uwezo wa kushinda msukosuko wa kumpoteza mama yake aliyefia shahidi akiwa bado mdogo.

Alipata utulivu na faraja ya kiroho kupitia kuhifadhi Qur’ani Tukufu. Alieleza kuwa uchungu wa kumpoteza mama yake shahidi ulimgeukia kuwa msukumo mkubwa wa kuendelea na safari ya kuhifadhi Qur’ani, safari iliyohitaji miaka ya juhudi endelevu na umakini mkubwa.

Msichana huyo alisema kuwa, baada ya msaada wa Mwenyezi Mungu, anautambua mchango wa mama yake mlezi, aliyempokea na kumpatia msaada wa kisaikolojia na kielimu aliouhitaji ili kuishinda hatua hiyo ngumu maishani mwake.

Alisisitiza kuwa msaada huo ulikuwa msingi uliomwezesha kuhifadhi Qur’ani nzima licha ya hali zote ngumu zinazoendelea kutawala katika Ukanda wa Gaza.

Aliongeza kuwa safari ya kuhifadhi Qur’ani nzima haikuwa rahisi, lakini azma yake ya kutimiza ndoto hiyo ilikuwa imara kuliko changamoto yoyote aliyokabiliana nayo wakati wa masomo na mafunzo yake. Alisisitiza kuwa Qur’ani Tukufu ilikuwa rafiki mwaminifu aliyeandamana naye wakati wa upweke na kumsaidia kuijenga upya maisha yake.

Habiba, pamoja na wahifadhi wengine 600 wa Qur’ani, walihudhuria hafla kubwa iliyofanyika hivi karibuni kwa ajili ya kutambua na kuenzi juhudi zao.

Tukio hilo linaonesha dhamira ya jamii ya waumini wa Gaza na taasisi za Kiislamu ya kuwaunga mkono vijana wenye vipaji ambao wameshikamana na njia ya ubora licha ya hali ngumu ya Gaza.

Mashirika yaliyoandaa hafla hiyo yaliwatuza vijana wahifadhi wa Qur’ani kutoka Gaza, kwa lengo la kuangazia mifano ya kuhamasisha ya watu wanaokabiliana na dhiki kwa matumaini.

Hafla hiyo ilihitimishwa kwa mahudhurio makubwa ya wazazi waliokuja kujivunia mafanikio makubwa ya watoto wao katika kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

3498477

Habari zinazohusiana
captcha