IQNA

Zaidi ya wanahabari 700 wanaakisi matembezi ya Arbaeen jijini Karbala

15:30 - August 03, 2026
Habari ID: 3482578
IQNA – Mbali na uwepo wa wanahabari 143 wa ndani na wanaharakati wa vyombo vya habari wanaohabarisha kuhusu matembezi ya Arbaeen, karibu wanahabari 600, wanaharakati wa vyombo vya habari, wapiga picha, na wafanyakazi wa kiufundi kutoka nchi mbalimbali wanashiriki katika kuangazia tukio hili adhimu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Serikali ya Karbala, Tawfiq Al-Habbali, ambaye ametangaza kukamilika kwa maandalizi maalum ya vyombo vya habari kwa ajili ya matembezi ya Arbaeen kwa kuzindua kituo cha habari kilicho na vifaa vya kisasa ili kutoa huduma kwa wanahabari wa ndani, wa Kiarabu, na wa kimataifa.

Katika mahojiano na Shafaq News, Al-Habbali amebainisha kuwa kituo hicho maalum cha habari cha Arbaeen kina jukwaa maalum kwa ajili ya matangazo ya moja kwa moja ya vipindi vya vyombo vya habari, huduma za intaneti, eneo maalum la kupumzika kwa wanahabari, na ufikiaji wa takwimu, namba, na taarifa sahihi zinazohusiana na tukio la Arbaeen.

Alieleza kuwa Utawala wa Karbala umesambaza magari 23 ya utangazaji wa satelaiti (SNG) katika jiji zima na barabara zinazoelekea humo, na vifaa 18 vya LiveU vimetolewa kwa vyombo vya habari kama msaada wa kilogistiki kwa ajili ya utangazaji wa moja kwa moja wa matukio hayo.

Al-Habbali amesisitiza kuwa Utawala wa Karbala unafanya kila juhudi kutoa vifaa na huduma zote muhimu za kiufundi na kilogistiki ili kuhakikisha mafanikio ya upeperushaji wa habari za tukio hili, kulingana na idadi kubwa ya mazuwar wanaohudhuria sherehe za Arbaeen.

Arbaeen ni tukio la kidini linalozingatiwa na Waislamu wa Kishia katika siku ya arobaini baada ya Siku ya Ashura, kuadhimisha kuuawa shahidi kwa Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na Imam wa tatu wa Kishia.

Hii ni moja ya mijumuiko mikubwa zaidi ya kila mwaka duniani, ambapo mamilioni ya Waislamu wa Kishia, pamoja na Ahul Sunna wengi na wafuasi wa dini nyingine, wanatembea kwa miguu kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Mwaka huu, siku ya Arbaeen itaangukia tarehe 4 Agosti.

3498503

captcha