iqna

IQNA

Wapalestina wawili wameuawa shahidi na wengine wanne wamejeruhiwa katika mashambulizi ya leo asubuhi ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza.
Habari ID: 1437512    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/09

Rais Rouhani
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Waislamu katika Ukanda wa Ghaza hatimaye watapata ushindi dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kwamba Iran daima itasimama pamoja mataifa yote yanayodhulimiwa wakiwemo Wapalestina, Wairaqi na Wasyria.
Habari ID: 1436787    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/06

Makubaliano ya muda ya usitishwaji vita yameanza kutekelezwa katika Ukanda wa Ghaza baada ya utawala ghasibu wa Israel kulazimika kukubali masharti ya wanamapambano wa Kipalestina ya kuondoa majeshi yake katika ukanda huo.
Habari ID: 1436767    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/06

Jeshi la utawala haramu wa Israel limeendeleza mauaji ya umati katika eneo la Ukanda wa Ghaza hii leo kwa siku ya 28 mtawalia na kuifanya idadi ya mashahidi wa hujuma hiyo kukaribia 2,000.
Habari ID: 1435964    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/04

Utawala wa Kizayuni wa Israel haujatosheka kwa kuwaua kwa umati wanawake na watoto wa Ghaza bali pia umeharibu kwa mabomu idadi kubwa ya misikiti na mahospitali katika ardhi hiyo ya Wapalestina.
Habari ID: 1435255    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/03

Wakati ulimwengu mzima ukionesha kusikitishwa na mauaji ya kinyama yanayofanywa na jeshi la Israel dhidi ya Wapalestina, maulama wa Saudia wameendelea kutoa fatuwa za kuwakandamiza Wapalestina.
Habari ID: 1435174    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/03

Huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukiendeleza jinai za kivita na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi wala hatia huko katika Ukanda wa Ghaza, Marekani imejitokeza wazi kuunga mkono kwa hali na mali jinai za utawala huo bandia.
Habari ID: 1435160    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/02

Duru za habari katika Ukanda wa Ghaza zinaarifu kuwa, karibu Wapalestina 1,700 wameshauawa shahidi katika jinai za siku 27 mtawalia za utawala huo katili wa Kizayuni kwenye ukanda huo.
Habari ID: 1435159    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/02

Imam Khamenei
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, 'ulimwengu wa Kiislamu kwa kuweka kando hilitalfu zilizopo, utumie uwezo wake wote kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.'
Habari ID: 1434650    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/29

Baada ya kumalizika muhula wa usitishwaji vita wa muda katika Ukanda wa Ghaza, utawala wa Kizayuni wa Israel umeanzisha tena hujuma zake za kinyama dhidi ya eneo hilo la Wapalestina.
Habari ID: 1433806    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/27

Ayatullah Sheikh Issa Qassim wa Bahrain amekosoa kimya cha baadhi ya nchi za Kiarabu kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 1433642    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/26

Hatimaye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Julai 20 lilivunja kimya chake na kudai kuwa linasikitishwa na idadi kubwa ya raia wanaouliwa na kujeruhiwa huko Ukanda wa Ghaza na kutaka kusimamishwa mara moja kile ilichokitaja kuwa ni uhasama.
Habari ID: 1432292    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/22

Idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika mashambulizi ya kikatili yaliyofanywa na jeshi vamizi la Israel katika eneo la Shujaiyya huko Ghaza imepindukia watu 100 na zaidi ya 200 wengine kujeruhiwa.
Habari ID: 1431786    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/21

Utawala haramu wa Israel umezidisha jinai zake dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi kwa kuanzisha hujuma ya kijeshi ya nchi kavu katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 1430956    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/19

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amezungumzia tukio la kusikitisha la kuuawa wananchi wa Ghaza hasa wanawake na watoto na kusisitiza kuwa, kadhia ya Ghaza kwa hakika ni ya kusikitisha na utawala wa Kizayuni wa Israel umeamua kutekeleza jinai kutokana na mghafala ulioko katika ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 1430240    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/16

Utawala haramu wa Israel unaendeleza jinai zake za kinyama katika Ukanda wa Ghaza ambapo mbali na kuwaua shahidi Wapalestina wakiwemo wanawake na watoto pia utawala huo umebomoa misikiti, nyumba, na mahospitali katika eneo hilo la Palestina.
Habari ID: 1429748    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/14