IQNA

Wazayuni wabomoa misikiti, waua shahidi Wapalestina Ghaza

16:50 - August 09, 2014
Habari ID: 1437512
Wapalestina wawili wameuawa shahidi na wengine wanne wamejeruhiwa katika mashambulizi ya leo asubuhi ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza.

Ashraf al Qudra msemaji wa kituo cha matibabu ya dharura cha Ukanda wa Ghaza amesema kuwa, ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zimezishambulia nyumba katika kambi ya wakimbizi ya Jabaliya bila ya kutoa tahadhari mapema na kuwajeruhi Wapalestina wanane wakiwemo watoto wadogo wawili.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vijana wawili wa Kipalestina wameuliwa shahidi katika mashambulizi ya ndege za kivita za utawala wa Kizayuni katika mashamba ya kilimo katika eneo la Diirul Balah katikati mwa Ghaza sambambab na kuzibomoa nyumba sita za raia katika maeneo mengine ya ukanda huo. Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni leo asubuhi pia zimeibomoa misikiti miwili katika kambi ya al Nusirat huko katikati mwa Ukanda wa Ghaza na msikiti mwingine katika eneo la al Zaitun.

1437316

Kishikizo: zaitun ghaza balah ndege
captcha