gaza - Ukurasa 18

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema hali katika Ukanda wa Ghaza inamkumbusha kuhusu hali ilivyokuwa katika nchi yake wakati wa utawala wa mfumo katili wa ubaguzi wa rangi maarufu kama Apartheid.
Habari ID: 3473925   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/19

Misikiti katika eneo la Ukanda wa Ghaza katika ardhi za Palestina imesafishwa kwa dawa za kuua virusi kabla ya kufunguliwa baada ya kufungwa kwa miezi miwili ili kuzuia kuenea kirusi cha corona.
Habari ID: 3473283   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/22

TEHRAN (IQNA)- Maandamano ya Siku ya Ardhi yalifanyika leo kwa siku ya nne mfululizo huko katika Ukanda wa Gaza na kushambuliwa tena na askari wa utawala ghasibu wa Israel.
Habari ID: 3471451   Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/02

TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Mataifa umeulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuzuia maendeleo pamoja na kuzorotesha hali ya kibinadamu katika ardhi za Palestina zilizo katika eneo la Quds Mashariki, Ukingo wa Maghribi na Ukanda wa Ghaza katika kipindi cha zaidi ya miaka 50 ya kukalia kwa mabavu maeneo hayo.
Habari ID: 3471173   Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/14

Katika hatua ya kushangaza, Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekataa kuuoredhesha utawala haramu wa Israel na ambao unaendelea kuua watoto wa Ukanda wa Gaza, katika orodha ya tawala zinazovunja haki za watoto duniani.
Habari ID: 3312923   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/10

Wakimbizi Wapalestina walio katika nchi mbali mbali duniani wanakabiliwa na matatizo makubwa sana. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetoa onyo kuhusu hali mbaya sana ya wakimbizi Wapalestina.
Habari ID: 3023920   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/03/22

Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, kumeundwa kamati ya uchunguzi kuhusiana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika ukanda wa Gaza.
Habari ID: 1472788   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/13

Ali Larijani
Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran yaani Bunge amesema , leo taifa la Iran linafakhari kuwa, kwa uwezo wake wote limeweza kulisaidia taifa la Palestina katika kipindi chake kigumu zaidi.
Habari ID: 1443997   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/28

Daktari Erik Fosse kutoka Norway ambaye yuko katika eneo la Ukanda wa Ghaza linalozingirwa na utawala haramu wa Israel kwa miaka kadhaa sasa, ameukosoa vikali utawala huo ghasibu kwa kutupa mabomu yenye kusababisha maradhi ya saratani dhidi ya wananchi wa Palestina walioko katika eneo hilo.
Habari ID: 1429754   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/14