IQNA

Ali Larijani

Iran ina fakhari kuwa imewasaidia Wapalestina wanaodhulumiwa

12:18 - August 28, 2014
Habari ID: 1443997
Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran yaani Bunge amesema , leo taifa la Iran linafakhari kuwa, kwa uwezo wake wote limeweza kulisaidia taifa la Palestina katika kipindi chake kigumu zaidi.

Ameongeza kuwa taifa la Iran lina fakhari kuwa kwa mara nyingine limetoa msaada na kuwezesha ushindi mkubwa kwa jihadi ya taifa linalodhulumiwa la Palestina.  Akizungumza Bungeni siku ya Jumatano, Larijani alisema kuwa, taifa madhlumu na shujaa la Palestina limeonesha kuwa kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu daima na mapambano wanaweza kuushinda utawala wa Kizayuni wa Israel wenye nguvu kubwa za kijeshi. Huku akiashiria makubaliano ya kudumu ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza, Larijani  aliongeza kuwa, baada ya vita vya kichokozi vya karibu miezi mwili vya Israel vilivyoungwa mkono kwa hali zote na Wamagharibi hasa Marekani, na ukimya wa baadhi ya nchi za Kiarabu hatimaye mapambano ya Palestina yamewafanya dhalili wafanya chochochoko wa Kizayuni.  Akilihutubu taifa la Palestina, Spika wa Bunge la Iran amesema kama tunavyonukuu, "Nyinyi Wapalestini ni lulu imara na madhubuti ya muqawama, na mashujaa msioweza kuelezeka kati ya lulu za mashujaa, na uwezo  huu kwa rehma za Mwenyezi Mungu utawezesha kuangamizwa tezi la saratani la utawala wa Kizayuni," Mwisho wa kunukuu.

1443612

captcha