Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA Afrika Mashariki, hafla hiyo ilianza Julai 20 na itanedelea kwa muda wa wiki moja.
Katika siku ya kwanza ya ‘Wiki ya Qur’ani kwa Hisani ya Iran’ ilianza kwa Qasida za kundi la ‘Taha’ katika Msikiti wa Ahul Bayt AS katika mji wa Jinja na pia katika Taasisi ya Imam Hussein AS katika eneo la Bugiri mashariki mwa Uganda ambapo klifanyika program kadhaa zinazohusiana na Qur’ani. Katika siku ya pili ya ‘Wiki ya Qur’ani Kwa Hisani ya Iran’ qarii wa kimataifa wa Qur’ani Tukufu kutoka Iran alisoma Qur’ani mbele ya hadhirina katika Madrassah ya Kinara ya Ahlul Sunna mjini Kampala baada ya sala ya adhuhuri. Aidha kulikuwa na kundi la Qasida katika hafla hiyo. Inatazamiwa kuwa qarii na hafidh wa kimataifa wa Qur’ani Tukufu kutoka Iran atashiriki katika programu kadhaa zitakazofanyika katika madrassa na televisheni mjini Kampala. Kundi la Qasida la ‘Taha’ kutoka Iran liko Uganda likiongozwa na Hussein Qorbani, qarii wa kimataifa wa Qur’ani. Kundi hilo liko Uganda kwa ushirikiano wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu na Idara ya Utamaduni ya Iran mjini Kampala na litakuwa nchini Uganda kwa muda wa wiki moja.
1432423