IQNA

Iran yaitaka jamii ya kimataifa izidi kuishinikiza Israel

18:21 - August 18, 2014
Habari ID: 1440685
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeitaka jamii ya kimataifa na hususan mashirika ya misaada ya kibinadamu kuushinikiza utawala wa Kizayuni uache kuuzingira Ukanda wa Ghaza na uruhusu misaada ya kibinadamu iwafikie wakazi wa ukanda huo uliozingirwa kila upande.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Bi Marzie Afkham amesema hayo leo na kuongeza kuwa, walimwengu wanafuatilia kwa masikitiko makubwa taarifa zinazohusiana na hali ya kusikitisha mno ya wakazi wa Ukanda wa Ghaza hususan hali mbaya ya masuala ya afya na tiba na namna majeruhi wanavyoteseka pamoja na kuripuka magonjwa mbalimbali kulikosababishwa na mashambulizi ya kikatili ya Wazayuni yaliyoharibu miundombinu ya ukanda huo.
Wakati huo huo Bi Valerie Amos, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Misaada ya Kibinadamu amesema kuwa, hatua zilizochukuliwa na Baraza la Usalama la umoja huo kuhusu kuondoa mzingiro wa Ghaza hazitoshi kabisa.
Bi Amos amesema hayo Jumapili mbele ya waandishi wa habari hapa mjini Tehran na kusisitiza kuwa, hatua zilizochukuliwa hadi hivi sasa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kuondoa mzingiro wa Ghaza hazitoshi kabisa licha ya kwamba umoja huo umetoa ushahidi wa nyaraka kuhusu madhara ya kuzingirwa ukanda huo kwa karibu miaka minane sasa.

1440368

Kishikizo: iran ghaza afkham palestina
captcha