Waziri Abdul Latif Siddique ametimuliwa kazi baada ya mashtaka yaliyowasilishwa na kundi la wanasheria wa Bangladesh kutokana na matamshi machafufu yaliyotolewa na waziri huyo dhidi ya matukufu ya Kiislamu.
Wakili wa Mahakama Kuu ya Bangladesh Yunus Ali amesema, kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo adhabu ya mtu anayehujumu itikadi za kidini za wananchi ni kifungo cha miaka 14 au kifungo cha maisha jela. Yunus Ali amesema atawasilisha mashtaka dhidi ya Abdul Latif Siddique.
Jumapili iliyopita waziri huyo wa zamani wa mawasiliano wa Bangladesh ambaye aliandamana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Sheikh Hasina mjini New York, Marekani alitoa matamshi machafu yaliyovunjia heshima ibada ya Hija, Waislamu na Mtume Muhammad (saw).
Katika sehemu moja ya matamshi yake Siddique alidai kwamba Waislamu wanaokwenda kuhiji katika Nyumba ya Mwenyezi Mungu huko Makka wanafuja na kuharibu pesa bure. Aliwataka maelfu ya Wabangali walioko Makka kwa ajili ya ibada ya Hija wawekeze fedha zao katika masuala ya kiuchumi badala ya safari ya Hija.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Bangladesh amedai kuwa safari hiyo ya Hija inayofanywa kila mwaka na Waislamu ni utaduni usio sahihi.
Abdul Latif Siddique ni mwanachama wa chama tawala cha Bangladesh.
1456496 AIR