Ayatullah Muhammad Ali Muvahhedi Kermani amesema kuwa, akiba bora zaidi ya mwanadamu katika maisha ya duniani na akhera ni kumcha Mwenyezi Mungu na kuongeza kwamba, uchaji Mungu haumpi mwanadamu fursa ya kubaki kwenye dhuluma, bali humfungulia njia ya kuelekea kwenye saada na ukamilifu.
Katika sehemu nyingine ya hotuba ya Sala ya Idul Adh'ha, Ayatullah Kermani ameeleza pia baadhi ya baraka zilizomo katika siku ya Arafa na kusema kuwa, nguvu ya siku ya Arafa ya kuondosha madhambi ni kubwa zaidi kuliko ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani, lakini baadhi ya waumini wameghafilika na baraka za siku hiyo na wala hawatambui umuhimu wake.../mh