IQNA

Mjumbe wa Rais Putin akutana na Sayyid Nasrallah

10:28 - December 07, 2014
Habari ID: 2615883
Mjumbe maalumu wa rais Vladimir Putin wa Russia amekutana na kufanya mazungumzo na katibu mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

Ripoti zinasema kuwa Mikhail Bogdanov Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia na mjumbe maalumu wa Rais Putin katika masuala ya Mashariki ya Kati amekutana na Sayyid Hassan Nasrallah mjini Beirut.
Hadi sasa hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu mazungumzo hayo.
Mjumbe huyo maalumu wa Russia aliwasili Beirut siku ya Ijumaa kwa lengo la kuadhimisha kumbukumbu ya kuanzisha uhusiano wa Lebanon na Russia.
Safari hiyo inahesabiwa kuwa na umuhimu mkubwa kwani Bogdanov ni mwanadiplomasia mwandamizi aliye karibu na Rais Vladimir Putin.
Gazeti la Daily Star la Lebanon limedokeza kuwa mwandiplomasia huyo wa Russia pia alijaribu kupatanisha pande hasimu kisiasa nchini humo.../mh

2615799

captcha