Azimio hilo lililopasishwa kwa pamoja na wanachama wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Myanmar kuwaruhusu Waislamu wa Rohingya ambao ni jamii ya wachache nchini humo kuwa na uhuru kamili na vile vile kuhakikisha vitendo vya utumiaji mabavu na ubaguzi dhidi ya wananchi hao vinakomeshwa. Taarifa ya Baraza Kuu la Umoja Mataifa imebainishwa kwamba, kupatiwa uraia kamili Waislamu wa Rohingya kutawafanya wawe na uhuru wa kutembea kwa kutembea katika maeneo yote ya nchi hiyo. Serikali ya Myamnar inawatambua Waislamu wa Rohingya kuwa ni wahajiri haramu kutoka nchi jirani ya Bangladesh na imekuwa ikikataa kuwapatia uraia kamili.../mh