IQNA

"Mashambulizi ya Paris hayana uhusiano na Uislamu"

16:03 - January 10, 2015
Habari ID: 2692011
Rais Francois Hollande wa Ufaransa amepinga kuweko uhusiano wowote kati ya wafanya mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo Paris na dini ya Kiislamu.

Akihutubia taifa jana Ijumaa, Rais wa Ufaransa amewataka wananchi wawe na umoja na kuchukua tahadhari kufuatia kujiri mashambulizi hayo yakuogofya huko Ufaransa. Rais Hollande amesema kuwa, wale wote waliohusika na mashambulizi ya Paris walikuwa ni watu wenye misimamo ya kuchupa mipaka wasio na mfungamano wowote na Uislamu. Katika hotuba yake ya jana kwa taifa, Rais wa Ufaransa amewasisitizia raia wa nchi hiyo kuwa macho na kuwa na umoja.

Rais Hollande amewataka wananchi kushiriki kwenye maandamano ya umoja yaliyopangwa kufanyika kesho kote nchini humo kulaani mashambulizi ya kigaidi ya Paris. Waislamu wa Ufaransa na katika maeneo mengine duniani wamelaani mashambulizi ya hivi karibuni katika mji wa Paris.../mh

2690786

captcha