IQNA

Diplomasia

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lalaani hujuma ya kigaidi nchini Iran

11:29 - August 17, 2023
Habari ID: 3477449
NEW YORK (IQNA)- Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa inayolaani shambulio la hivi karibuni la kigaidi katika Haram Takatifu ya Hadhrat Ahmad bin Musa (AS) maarufu kama Shah Cheragh mkoani Fars kusini mwa Iran.

Katika taarifa yao hapo jana, nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zililaani shambulio hilo la kigaidi na la uoga dhidi ya watu wasio na hatia yoyote na mazuwari wa Haram ya Shah Cheragh.

Kadhalika nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zimesisitiza kwamba, hatua ya kigaidii ya aina yoyote iile na inayofanyika kwa msukumo na malengo yoyote yale katu haikubaliki kwa namna yoyote ile. 

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo sambamba na kutoa mkono wa pole kwa serikali, wananchi na familia za wahanga na mashahidi wa shambulio hilo imesisitiza juu ya udharura wa kuwajibika wale wanaowasaidia kifedha magaidi pamoja na waungaji mkkono wao.

Siku ya Jumapili, gaidi kutoka Tajikistan aliendesha ufyatuaji risasi katika haram ya Shah Cheragh, na kuua shahidi watu wawili na kujeruhi watu saba. Gaidi mmoja alikamatwa papo hapo na kukabidhiwa kwa vyombo vya sheria. Kundi la kigaidi la Daesh limedai kuhusika na shambulio hilo la kigaidi.

Ikumbukwe kuwa, mnamo Oktoba 26 mwaka jana (2022), gaidi mwenye silaha aliingia ndani ya eneo hilo la ibada, na kuwaua wafanyaziara 15, wakiwemo wanawake na watoto, na kujeruhi wengine kadhaa kabla ya kupigwa risasi na kujeruhiwa na vikosi vya usalama. Gaidi huyo baadaye alifariki dunia hospitalini kutokana na majeraha aliyopata.

3484816

captcha