Shambulio hilo lilitokea eneo la Kurram, wilaya katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa.
Hakuna aliyedai mara moja kuhusika na shambulio la hivi karibuni, lakini mashambulizi sawa na hayo yamekuwa yakitekelezwa na magaidi wakufurishai ncini humo.
Hujuma hiyo imekuja wiki moja baada ya mamlaka kufungua tena barabara kuu katika eneo hilo ambayo ilikuwa imefungwa kwa wiki kufuatia mapigano makali.
Afisa wa polisi wa eneo hilo Azmat Ali alisema magari kadhaa yalikuwa yakisafiri katika msafara kutoka mji wa Parachinar kuelekea Peshawar, mji mkuu wa Khyber Pakhtunkhwa, wakati watu wenye silaha walipofyatua risasi. Alisema takriban abiria 10 wako katika hali mbaya hospitalini.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mohsin Naqvi alisema takriban watu 38 waliuawa katika "shambulio la kigaidi." Waziri Mkuu Shehbaz Sharif na Rais Asif Ali Zardari walilaani shambulio hilo, na Sharif alisema wale waliohusika na mauaji ya raia wasio na hatia hawataadhibiwa.
4249707