Akihutubu hivi karibuni, Rais wa Ghana amesema anafungamana na utekelezwaji wa kifungu cha 21 katika katiba ya nchi ambacho kinawapa raia uhuru wa kuabudu.
'Ni kinyume cha katiba kuwalazimu wanafunzi Waislamu kuenda kanisani au wanafunzi Wakristo kulazimishwa kuenda msikitini', amesema Rais wa Ghana. Aidha amesema, 'Si sahihi kuwazuia wanawake Waislamu kuvaa Hijabu au kuwazuia watawa wa kike kikatoliki kuvaa vazi lao.' Halikadhalika ametoa onyo kali na kusema kuwa yeyote atakayepuuza agizo hilo la kikatiba atachukuliwa hatua. Tamko hilo la Rais Mahama wa Ghana limekuja baada ya kujiri vitendo kadhaa vya wanafunzi Waislamu katika shule za upili na wanawake Waislamu katika sekta ya umma kulazimishwa kuvua vazi lao la Hijabu. Vitendo hivyo vya kuwabagua wanawake Waislamu hasa hujiri katika shule na vyuo vinavyosimamiwa na wamishonari Wakristo.
Waislamu nchini Ghana wamemshukuru na kumpongeza Rais Mahama tamko lake hilo....mh