Yang Hi Li, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa hali waliyo nayo Waislamu wa kabila la Rohingya wa Myanmar waishio makambini ni mbaya sana. Li amebainisha hayo Jumatatu hii wakati alipokuwa anahutubia kikao cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi. Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa vitendo vya ubaguzi wa kidini dhidi ya jamii ya walio wachache katika jimbo la Rakhin huko Myanmar zimeshamiri sana. Yang Hi Li amesema kuwa kuna uadui na chuki kubwa sana kati ya makundi ya kikabila na kidini huko Myanmar na kwamba hadi sasa hakujafanyika uchunguzi wowote thabiti kuhusiana na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa dhidi ya Waislamu wa kabila la Rohingya katika miaka ya 2012 na 2014.../mh