Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Reza Golshahi ataiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kitengo cha qiraa au kusoma huku Mohammad Ali Islami akishiriki katika kitengo cha kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu.
Wawili hao walishika nafasi za kwanza katika mashindano ya kitaifa ya Qur’ani nchini Iran.
Mwaka jana Iran pia ilituma washiriki katika mashindano hayo ambapo, Mahmoud Nouruzi alipata nafasi ya tatu katika qiraa huku Peyman Ayazi akishika nafasi ya nne katika hifdhi.
Iran hutuma washiriki katika mashindano ya kimataifa ya kuhifadi na kusoma Qur’ani tukufu na aghalabu hushika nafasi za juu. Katika miaka ya hivi karibuni Iran imeimarisha harakati za Qur’ani katika jamii hasa miongoni mwa vijana.../mh