Sheikh Khalid Al Mulla ameongeza kuwa kupambana na kundi la kigaidi la Daesh hivi sasa ni jambo la faradhi. Akiashiria jinai za kundi la Daesh katika ulimwengu wa Kiislamu amesema: "Matakfiri wa Daesh wanausambaratisha umma wa Kiislamu hivyo tuna wajibu wa kulizuia kundi hili."
Katika ukurasa wake wa kijamii wa Facebook, Sheikh Al Mullah amesisitiza kuhusu udharura wa kupambana na Daesh na kusema: "Vita dhidi ya wafuasi wa Daesh popote pale duniani ni wajibu matakatifu na wa kisheria kwani lengo ni kuilinda dini, mali, familia, roho na mantiki."
Mwenyekiti wa Maulamaa wa Ahlul Sunna nchini Iraq ametoa wito kwa Wairaqi wasihadaiwe na magaidi wa Daesh kwani dalili wanazotoa hazina mantiki. Ameongeza kuwa magaidi wa Daesh wanawapiga vita Waislamu wawe ni Mashia au Masunni.../mh