IQNA

Wauaji wa Sheikh Shehata Misri wapata kifungo hafifu gerezani

11:30 - June 14, 2015
Habari ID: 3314097
Mahakama moja nchini Misri imewahukumu kifungo hafifu cha miaka 14 jela watu 23 waliokuwa wanatuhumiwa kwa kutekeleza mauaji dhidi ya Waislamu wanne wa Kishia hapo mwezi Juni mwaka 2013 nchini humo.

Aidha watu wengine wanane waliokuwa wakituhumiwa kupanga njama za kufanya mauaji na kuchoma nyumba moja wameachiliwa huru na mahakama hiyo. Waislamu hao wanne waliouawa ni pamoja na Allamah Hassan Shehata mmoja wa wasomi wa Kishia, aliyeuawa pamoja na wenzake watatu mwezi Juni mwaka 2013, baada ya kundi la Kiwahabi kushambulia kijiji kilicho katika kiunga cha Cairo, mji mkuu wa nchi hiyo. Mwezi Februari, mahakama ya jinai ya mjini Giza, iliakhirisha kesi hiyo sanjari na kuwarejesha rumande watuhumiwa 31. Awali idadi kadhaa ya wanasiasa na wataalamu wa sheria nchini Misri, waliitaka mahakama ya nchi hiyo kutoa hukumu haraka dhidi ya wahusika wa mauaji ya Allamah Hassan Shehata kwa lengo la kuzuia kukaririwa tukio kama hilo katika jamii ya Wamisri. Aidha mauaji ya Waislamu hao wa Kishia yalikosolewa na asasi mbalimbali za ndani na nje ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.../mh

3314055

Kishikizo: shehata misri kifo shia
captcha