Haji-Hassani Kargar aliyechukua nafasi ya kwanza katika kitengo cha qiraa cha mashindano hayo amesema Iran imeweza kupiga katika katika masuala ya Qur'ani kama vile qiraa kutokana na baraka za uongozi wenye busara wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ambaye kwa hakika ni Ustadhi mkubwa wa Qur'ani katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Haji-Hassani Kargar ameyasema hayo katika mahojiano na waandishi habari pembizoni mwa sherehe za kufunga mashindano ya ya Qur'ani nchini Malaysia.
Akijibu swali kuhusu kiwango cha mashindano hayo ya Qur'ani, amepongeza kiwango chake cha juu hasa cha washiriki kutoka Misri, Indonesia na Malaysia.
Mashindano ya 57 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Malaysia yalianza Jumanne wili iliyopita na kuendelea kwa siku tano kwa kuwaleta pamoja washiriki kutoka nchi 70.../mh