Waumini kutoka mji wa Quds na Ukingo wa Magharibi walianza kumiminika katika msikiti wa Al Aqsa kuanzia Ijumaa alfajiri. Mamia ya askari wa utawala ghasibu wa Israel walisambazwa katika milango yote ya msikiti huo. Polisi waliwazuia wanaume Wapalestina walio chini ya umri wa miaka 40 kuingia katika msikiti huo.
Baada ya sala ya Ijumaa, mamia ya waumini waliandamana kufungamana na Khader Adnan Mpalestina aliyesusia kulak wa muda wa siku 52 sasa katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Al Aqsa ni sehemu ya tatu kwa utukufu katika Uislamu baada ya Misikiti ya Makka na Madina.
Hivi karibuni Mkuu wa Kamati Kuu ya Kiislamu ya Palestina amewataka Waislamu wahudhurie kwa wingi katika msikiti mtukufu wa al Aqsa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Sheikh Ekrima Sa'id Sabri alitangaza kuwa ni wajibu kwa Waislamu na hasa Wapalestina kuitumia fursa wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuhudhuria muda wote katika msikiti wa Al Aqsa ili kukabiliana na njama za Wazayuni.../mh