IQNA

1,000 Waliohifadhi Qur’ani Ghaza waenziwa

17:17 - July 07, 2015
Habari ID: 3325720
Taasisi ya Dar-ul-Qur’an na Sunnah katika Ukanda wa Ghaza imewaenzi wakaazi 1000 wa eneo hilo walio hifadhi Qur’ani kikamilifu.

Kwa mujibu wa tovuti ya al-Sharq, hafla ya kuwaenzi mahufadh hao ilifanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Rashad al Shawa huko Ghaza kwa ushirikino wa Taasisi ya Misaada ya Eid ibn Muhammad Al Thani.
Waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Sheikh Hassan Al-Laham, Mufti wa Ghaza, Sheikh Abdullah ibn Sulayman Al-Misri, Taasisi ya Dar-ul-Qur’an na Sunnah, Sheikh Abdul Basit Al-Satl na maustadh kadhaa wa Qur’ani Tukufu.
Maafisa wa Dar-ul- Qur’an wamewashukuru wote waliounga mkono miradi ya Qur’ani katika kituo hicho.
Eneo la Ghaza limekuwa chini ya mzingiro wa kinyama wa utawala wa Kizayuni kuanzia mwaka 2007. Aidha utawala wa Kizayuni umehujumu kijeshi eneo hilo mara kadhaa ambapo maelfu ya Wapalestina wameuawa  shahidi waengi wao wakiwa ni wanwake na watoto. Pamoja na kukumbana na masaibu hayo, Wapalestina katika eneo hilo wamesimama imara kwa imani yao huku wakiendeleza mapambano dhidi ya utawala katili wa Israel.../mh

3325386

Kishikizo: palestina ghaza qur'ani
captcha