Kwa mujibu wa tovuti ya El Nailein, Sheikh Mohammad Othman Salih, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Maulamaa wa wa Kiislamu Sudan ametoa taarifa na kutangaza bayana kuwa, “Makundi yenye misimamo mikali ambayo yanamwaga damu ya watu wasio na hatia duniani kwa jina la dini kwa hakika yanatenda jinai kubwa sana na ni haramu kujiunga na makundi kama hayo.”
Kuhusu hatua ya baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu Sudan kujiunga na kundi la kigaidi la Daesh au ISIS, amesema, “wanafunzi hao wamepata fikra potofu nje ya nchi na wamepotea njia.“
Sheikh Mohammad Othman Salih ameongeza kuwa Baraza Kuu la Maulamaa wa wa Kiislamu Sudan wataendeleza jitihada za kupambana na wenye misimamo mikali ya kidini. Amesema, “Sisi tunafanya kila tuwezalo ili kutoa mafunzo sahihi ya kidini kwa wananchi ili tukabiliane na wale wenye misimamo mikali.”.../mh