IQNA

Waislamu milioni 4 wameuawa katika vita vya Marekani-NATO

19:14 - August 23, 2015
Habari ID: 3350564
Inakadiriwa kuwa Waislamu wasiopungua milioni nne wameuawa katika miongo ya hivi karibuni Mashariki ya Kati katika vita vilivyoanzisha na madola ya maghairbi hasa Marekani na Marekani na Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO.

Katika ripoti maalumu, tovuti ya Global Research imehoji kuwa, kwa kuzingatia kuwa aghalabu ya waliouawa ni wenye asili ya Kiarabu na Waislamu, je itakuwa sawa kusema Marekani na waitifaki wake wametekeleza mauaji ya kimbari?  Kundi la ‘Madaktari Wenye Kuwajibika Kijamii’ katika ripoti ya mwezi Machi mwaka huu walisema watu waliopoteza maisha katika vita vya Iraq vilivoanza mwaka 2003 ni milioni 1.3 hadi milioni 2. Aidha ripoti hiyo imesema, ‘waliouawa katika vita maeneo mengine Mashariki ya Kati ni zaidi, na idadi hiyo inaweza kufika milioni 4 kwa kuzingatia waliouawa katika nchi zingine za eneo mbali na Iraq na Afghanistan.’ Ripoti hiyo pia imesema idadi hiyo inaweza kuongezeka kwa kuzingatia vikwazo dhidi ya Iraq vilivopelekea watu takribani milioni 1.7 kupoteza maisha karibu nusu yao wakiwa ni watoto. Vikwazo dhidi ya Iraq vilianza mwaka 1990 na kuendelea hadi mwaka 2003.

Maana ya 'mauaji ya kimbari'
Tovuti hiyo inasema kwa kuzingatia maana ya neno ‘Mauaji ya Kimbari’ kama ilivyoainishwa mwaka 1943, mbali na kuua watu, halikadhlika kuna vitendo vingi ambavyo vinahesbaiwa kuwa mauaji ya kimbari kama vile kukukusida makusidi kuangamiza kikamilifu au sehemu ya taifa, kundi la kidini au kundi la watu kwa rangi yao n.k. Ingawa ufafanuzi fasaha haujapatikana, kutokana na tofauti kati ya wataalamu wa mauaji ya kimbari, ufafanuzi wa kisheria hupatikana katika Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari (unaofupishwa "CPPCG" katika lugha ya Kiingereza) wa Umoja wa Mataifa wa mwaka wa 1948. Ibara ya 2 ya mkataba huo inayafafanua mauaji ya kimbari kama "Tendo lolote kati ya yale yafuatayo linalofanyika kwa nia ya kuharibu, kikamilifu au katika sehemu, kikundi cha kitaifa, kikabila, kirangi au cha kidini, kama vile: mauaji ya watu wa kikundi hicho; kusababisha athari kubwa upande wa mwili au wa akili kwa watu wa kikundi hicho; kutwika kwa makusudi juu ya kundi hali za maisha, zinazonuiwa kuleta uharibifu wa mwili mzima au sehemu ya mwili; kuchukua hatua zinazonuiwa kuzuia wanawake wasijifungue katika kikundi hicho; [na] kuhamisha watoto wa kikundi hicho hadi kikundi kingine kwa lazima.

Bush atangaza vita vya msalaba
Ripoti hiyo imesema baada ya Rais George W Bush wa Marekani kutangaza kile alichokiita ni “vita dhidi ya ugaidi’ mwaka 2001 baada ya matukio ya Septemba 11, huo ulikuwa mwanzo wa mauaji ya kimbari ya Waislamu. Hii ni kwa sababu  alitumia ibara kama vile ‘kuwaangamiza watenda maovu duniani’ na ‘vita vya msalaba dhidi ya ugaidi, ambavyo vitadumu muda mrefu.’ Ikumbukwe kuwa katika vita vya msalaba milienia moja iliyopita, majeshi ya Kikristo yalivamia na kuteka maeneo matakatifu kutoka kwa Waislamu. Kutimika ibara hiyo katika zama hizi kuna maana ya hujuma ya kiutamaduni na kiuchumi ya nchi za Magharibi dhidi ya mataifa ya Kiislamu. Kwa msingi huo Waislamu wana hofu kuwa vita hivyo vinalenga kuwaangamiza, kuwadhoofisha, kuwadhalilisha na kuuvunjia heshima Uislamu.
Katika vita vya Afghanistan na Iraq si tu kuwa Marekani iliwaangamiza kwa umati mamilioni bali iliharibu pia miundombinu ya kiafya na maisha katika nchi hiyo. Baada ya hapo Marekani sasa inafaidika katika kuhusisha mashirika yake katika ujenzimpya wa miundo mbinu hiyo na hivyo watu wa nchi hizo wanaendelea kubakia masikini. Hivi sasa pia kuna ushahidi kuwa Marekani inaendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu kwa kuunga mkono kundi la kigaidi la Daesh au ISIS katika nchi za Iraq na Syria.
Hivi sasa pamoja na kuwa Waislamu wanauawa kwa umati na Marekani na waitifaki wake kwa njia ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja, propaganda zinaenezwa duniani dhidi ya Uislamu na Waislamu kiasi kwamba baadhi ya watu katika nchi za Magharibi na hata zisizo za kimagharibi wanasisitiza ulazima wa kunyanyaswa, kudhulumiwa na kuuawa zaidi kwa umati Waislamu.../mh

3350363

captcha