IQNA

Watu 10 wauawa CAR baada ya wanamgambo wa Kikristo kuwahujumu Waislamu

18:40 - August 24, 2015
Habari ID: 3351057
Watu 10 wameuawa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) baada ya wanamgambo wa Kikristo kuwashambulia Waislamu. Imearifiwa kuwa mapigano hayo yamejiri katika eneo la Bambari, lenye Waislamu wengi, katikati mwa nchi hiyo lililo karibu na Mto Ouaka.

Mapigano hayo yaliibuka baada ya kundi la vijana wa Kikristo wanaotajwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi na lenye misimamo ya kufurutu ada la Anti-Balaka, kumuua kijana wa Kiislamu ambapo Waislamu nao waliamua kulipiza kisasi kwa mauaji hayo.
Hii si mara ya kwanza kujiri mapigano kama hayo ambayo yanatajwa kuchochewa na askari wa kigeni kutoka nchini Ufaransa.
Ikumbukwe kuwa hapa kwamba, Jamhuri ya Afrika ya Kati yenye jamii ya watu karibu milioni nne na laki nne, ilikuwa chini ya mkoloni Mfaransa, huku ikipata uhuru wake mnamo mwaka 1960. Duru za kuaminika, zinawataja askari wa Ufaransa kuwa, ndio ambao wamekuwa wakiendesha vitendo vya uchochezi baina ya raia wa taifa hilo, uchochezi ambao hadi sasa umepelekea maelfu ya watu kuuawa, wengi wao wakiwa ni Waislamu..../mh

3350144

Kishikizo: waislamu afrika KATI balaka
captcha