IQNA

Kundi la kigaidi la ISIS laweka sheria kali kwa mahujaji

14:07 - August 31, 2015
Habari ID: 3354583
Kundi la kigaidi la ISIS au Daesh limeweka sheria kali kwa wakaazi wa mji wa Mosul, Iraq ambao wanataka kuelekea katika safari ya kila mwaka ya ibada ya Hija.

Kundi la kigaidi la ISIS au Daesh limeweka sheria kali kwa wakaazi wa mji wa Mosul, Iraq ambao wanataka kuelekea katika safari ya kila mwaka ya ibada ya Hija. Kwa mujibu wa sheria hizo za ISIS, Waislamu wote wanaoelekea Hija wanalazimika kukabidhi kundi hilo la kigaidi mali zao zote pamoja na usimamizi wa familia zao. Kwa mujibu wa ripota wa televisheni ya TRT Türk ya Uturuki, ISIS imeweka sheria hizo ambazo zinakinzana na mafundisho ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa sheria hizo za kundi la kigaidi na la wakufurishaji la ISIS, baada ya mahujaji kukabidhi mali na familia zao, iwapo hawatarejea Mosul basi wasahau mali na familia zao.
Imearifiwa kuwa aghalabu ya mahujaji kutoka Mosul watapitia mkoa wa Al Anbar na kuingia Jordan kisha kuelekea Saudia kwa ajili ya Ibada ya Hija.
Kundi la kigaidi la ISIS limepotosha mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu na hutegemea itikadi za Kiwahabi. Magaidi hao wa ISIS wanatekeleza mauaji ya umati dhidi ya Mashia, Masuni na Wakristo katika maeneo wanayoyashikilia Iraq na Syria. Aidha magaidi hao wakufurishaji wanaendelea kubomoa idadi kubwa ya misikiti, kumbi za ibada, makaburi na turathi za kale katika maeneo wanayoshikilia.

captcha