IQNA

Maulamaa wa Saudia wapinga filamu ya Mtume Muhammad SAW

12:05 - September 06, 2015
Habari ID: 3358540
Baraza la Maulamaa katika utawala wa Saudi Arabia wametangaza kuipinga filamu ya Mtume Muhammad SAW iliyotengenezwa Iran.

Katika taarifa, baraza hilo limetaka filamu hiyo ipigwe marufuku kwa madai yasiyo na msingi kuwa eti inamvunjia heshima Mtume SAW na masahaba zake.
Baraza la Maulamaa ni taasisi muhimu zaidi ya kidini katika ufalme wa Saudia na humshauri mtawala wa nchi hiyo kuhusu masuala ya kidini. Baraza hilo la maulamaa wa Kiwahabi katika hatua ya kushangaza limewataka Waislamu wasiitizame filamu hiyo.
Hii ni katika hali ambayo Waislamu kote duniani wamepongeza kutengenezwa Filamu ya Muhammad SAW na kusema filamu hiyo itakuwa na nafasi muhimu katika kukabiliana na wale wenye chuki dhidi ya Uislamu. Aidha maulamaa wa Kiislamu maeneo mbali mbali duniani wameunga mkono filamu hiyo.
Filamu hiyo ya dakika 171 imetengenezwa kwa bajeti ya dola milioni 50 na imetajwa kuwa filamu iliyogharimu kiasi kikubwa zaidi cha fedha nchini Iran na kwamba ilichukua miaka mitano kuitengeneza.
Filamu hiyo iliyotengenezwa na mtengeneza filamu mashuhuri wa Iran Majid Majidi ni sehemu ya kwanza ya sehemu tatu kuhusu maisha ya Mtume SAW. Filamu hiyo ilianza kuoneyshwa Iran Agosti 27 na pia siku hiyo hiyo ikaonyeshwa katika Tamasha la Kimataifa la Filamu la Montreal nchini Canada.
Majidi amesisitiza kuwa filamu ya Mtume Muhammad SAW imezingatia sheria za Kiislamu kwani sura ya Mtume Mtukfuu haijaonyeshwa katika filamu hiyo.../mh

3358247

captcha