IQNA

Utamaduni

Tamasha la Kimataifa la Filamu za Kiislamu linafaniyika Tatarstan

21:20 - September 08, 2024
Habari ID: 3479399
IQNA - Toleo la 20 la Tamasha la Kimataifa la Filamu za Kiislamu la Kazan lilianza katika mji mkuu wa Jamhuri ya Tatarstan ya Shirikisho la Russia siku ya Ijumaa.

Katika sherehe za ufunguzi, mkuu wa idara ya utamaduni wa Waislamu wa Russia Roshan Abbasov alisoma ujumbe kutoka kwa Sheikh Ravil Gaynutdin, mkuu wa Baraza la Mamufti wa Russia.

Katika ujumbe wake, Sheikh Gaynutdin alipongeza tamasha hilo kwa kuunda fursa ya maingiliano kati ya dini na kuwaunganisha wasanii wa filamu kutoka nchi za Russia na Kiislamu katika kukuza akhlaqi njema na maadili ya kiroho na mawazo kwa amani na ubinadamu.

Abbasov pia alihutubia sherehe hiyo, akisema kwamba filamu zilizo na ujumbe wa kiroho na maadili na maadili ya kitamaduni ya ulimwengu zinavutia wengi katika jamii ya leo.

Aliongeza kuwa Tamasha la Kimataifa la Filamu za Kiislamu la Kazan limegeuka kuwa jukwaa la elimu, maendeleo ya kiroho na kuimarisha amani kupitia sanaa ya sinema.

Alibainisha kuwa tamasha hilo pia linajumuisha filamu za kundi la nchi za BRICS, na kuongeza kuwa mwaka 2024, wakati Russia ikishikilia urais wa zamu wa kundi hilo, jiji la Kazan limekuwa mwenyeji na linapanga kuandaa matukio mengine ya nchi za BRICS, yakiwemo mashindano ya michezo na mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.

Tamasha la Kimataifa la Filamu za Kiislamu la Kazan limefanyika kwa kauli mbiu "Kupitia Mazungumzo ya Tamaduni hadi Utamaduni wa Mazungumzo" tangu 2005.

Toleo la kwanza liliandaliwa chini ya mpango wa Baraza la Mamufti wa Russia, Shirika la Utamaduni na Sinema la Shirikisho la Russia, na Wizara ya Utamaduni ya Jamhuri ya Tatarstan kwa msaada wa mkuu wa Jamhuri ya Tatarstan.

Inafanyika kila mwaka kwa ushiriki wa makumi ya nchi, ikiwa ni pamoja na mataifa ya Kiislamu, ambapo  filamu zinazokuza maadili ya kiroho na akhlaqi njema huonyeshwa

Hafla ya mwaka huu imehudhuriwa na wasanii na wategeneza filamu kutoka Russia, Iran, Kazakhstan, Uturuki, Uzbekistan, Tajikistan, Algeria, Bangladesh, India, Pakistan, Sri Lanka, Nepal, Morocco, Senegal, China, Malaysia, Misri, Iraq, Oman, Mauritania, Tunisia, Cuba, Saudi Arabia, Uswizi, Oman, New Zealand, Argentina na Japan.

3489798

Habari zinazohusiana
captcha